Orodha Mafisadi wa Elimu Tanzania na Msemakweli

Hiki ni kitabu kipya kilichoandikwa na Msemakweli Kainerugamba. Kati ya mambo mengine mwandishi anatoa orodha ya majina ya watu vyeti bandia. Baadhi ya “mafisadi wa elimu” ni viongozi wakubwa serikalini. Mfano ni Makongoro Mahanga ambaye tayari ameshakwenda mahakamani kudai fidia kwa kudhalilishwa na Msemakweli. Taarifa kutoka kwenye mtandao, wengine ndani ya kitabu hicho ni Lukuvi, Mary Nagu, Kamalla,Diallo na Nchimbi.

Tanzania Commission of Universities (TCU)  jana wametoa tamko juu ya orodha hiyo. Prof  Nkunya akiongea na vyombo vya habari aliwataka wote walioandikwa wapeleke vyeti vyao TCU kwa uhakiki na udhibitisho kama ni halali au bandia.

Kwa sasa kati ya mambo yanayosubiriwa ni hao wahusika kupeleka vyeti vyao TCU na nini tamko la TCU juu ya uhalali wa vyeti husika.

Msemakweli kama Mwanasheri na mwandishi naona yeye ametimiza wajibu wake kuutarifu umma. Kazi ni kwa mahakama na walalamikaji kudhibitisha kwamba vyeti vyao ni halali. Swala la vteti feki, kwa kweli limechukua muda mrefu kushughulikiwa na serikali. Bado yapo maswaliya msingi yatakiwa majibu. Iweje TCU mpaka kitabu kitoke ndio wao wawatake washutumiwa kupeleka vyeti vyao kwa ukaguzi? Je hii sio “reactive management” wakati kwa taasisi nyeti kama yao walipaswa kuwa na “proactive management”.

Binafsi bado sijapata nafasi ya kukisoma kitabu hicho. Kwa wenye taarifa juu ya upatikanaji wake tafadhali mtujulishe.

Published in: on February 12, 2010 at 7:53 am  Leave a Comment  
Tags:

The URI to TrackBack this entry is: https://marafikiwavitabu.wordpress.com/2010/02/12/orodha-mafisadi-wa-elimu-tanzania-na-msemakweli/trackback/

RSS feed for comments on this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: