TCU yatahadharisha utapeli usajili Wanafunzi vyuoni

From Subi of http://www.wavuti.com

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewatahadharisha wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini juu ya kuwepo matapeli wanaowaomba pesa wanafunzi ili wawape matokeo ya udahili.

Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Profesa Mayunga Nkunya alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wakati shughuli ya udahili ikiendelea wamegundua kuwepo na matapeli ambao hutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa wanafunzi na kuwaomba fedha. Matapeli hao wamekuwa wakiwatumia wanafunzi ujumbe huo na kuwataka watume kiasi fulani cha fedha ili waweze kupewa matokeo ya udahili.

“Tunawatahadharisha wazazi na wanafunzi wote walioomba udahili wasitoe fedha yoyote kwa ajili ya kupata matokeo ya udahili kwani matokeo bado hayajatoka,” alisema Profesa Nkunya.

Alisema kuanzia mwaka wa masomo 2010/ 2011 tume hiyo, ilianzisha utaratibu mpya wa udahili wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kupitia mfumo wa udahili wa pamoja (CAS).

Katibu Mtendaji huyo alisema kufuatia utekelezaji wa mfumo huo, mchakato wa kudahili wanafunzi unapitia hatua mbalimbali ili kuwezesha waombaji wote kupata nafasi sawa kulingana na maombi yao kwa kutilia mkazo usawa na usahihi wa udahili huo. Alisema shughuli hiyo imechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kutokana na sababu mbalimbali na kulingana na upya wa mfumo wenyewe.

Nkunya alisema matokeo ya udahili yanatarajiwa kutolewa Septemba mwaka huu na kwamba hakutakuwa na malipo yoyote yatakayohitajika ili kupata matokeo hayo. Tume hiyo imewataka wazazi wote na wanafunzi walioomba udahili kupitia mfumo mpya wa udahili kutoa taarifa pindi watakapopokea ujumbe wowote unaowaomba fedha kwa ajili ya kupata matokeo ya udahili.

credit source: http://www.wavuti.com/4/post/2010/08/tcu-yatahadharisha-utapeli-usajili-wa-wanafunzi-vyuoni.html#ixzz0xgr1jYNF
Published in: on August 26, 2010 at 9:18 am  Leave a Comment  
Tags:

The URI to TrackBack this entry is: https://marafikiwavitabu.wordpress.com/2010/08/26/tcu-yatahadharisha-utapeli-usajili-wanafunzi-vyuoni/trackback/

RSS feed for comments on this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: